YANGA YAZUIWA KUFANYA MAZOEZI UWANJA WA TAIFA
Na Salum Fikiri. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga Sc, leo imezuiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam tayari kabisa kujiandaa na mchezo wao wa Ligi ya mabingwa barani Afrika. Yanga itacheza na St Louis wa Shelisheli Jumamosi ijayo kwenye uwanja huo wa Taifa lakini ikiwa katika maandalizi yake kama zimemavyo sheria za mashindano mwenyeji hupata wasaa wa kufanya mazoezi katika uwanja husika kabla ya kuwapisha wageni wao siku moja kabla ya mchezo imejikuta ikizuiwa. Nsajigwa Gordon ambaye ni meneja wa uwanja huo ameizuia Yanga isifanye mazoezi katika uwanja huo kwa madai kuwa bado uwanja huo haukidhi viwango vya timu kufanyia mazoezi hapo isipokuwa kuna ruhusa ya mechi, lakini hata hivyo St Louis wameruhusiwa kuutumia kwa kesho wakati Yanga wakalazimika kwenda kukodi uwanja mwingine kufanya mazoezi yao. Ikumbukwe kuwa Yanga ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, na kwa kitendo cha kuwanyima uwanja kinachukuliwa kama cha...