YANGA NA MAJIMAJI KUPIGWA SONGEA 16 BORA KOMBE LA FA
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Yanga Sc itasafiri tena hadi mjini Songea mkoani Ruvuma kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 16 Bora ya michuano ya Azam Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji Majimaji katika droo iliyopangwa leo kwenye studio za Azam Tv zilizopo Tabata Dar es Salaam.
Mechi zote za hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) zitafanyika kati ya Februali 22 na 25 mwaka huu na mbali ya Yanga kwenda Songea, vigogo wengine AzamnFc watamenyana na KMC ya Kinondoni mjini Dar es Salaam.
Wakati mkoa wa Shinyanga utahodhi mechi mbili mfululizo, ya kwanza ni Stand United na Dodoma Fc na baadaye Buseresere na Mtibwa Sugar uwanja wa Kahama.
Mechi nyingine za hatua hiyo ni JKT Tanzania na Ndanda Fc uwanja wa Mbweni Dar es Salaam, Kiluvya United na Tanzania Prisons, uwanja wa Filbert Bayi mjini Kibaha, Pwani, Singida United na Polisi Tanzania uwanja wa Namfua mjini Singida na Njombe Mji Fc itaumana na Mbao Fc uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Ikumbukwe Yanga na Majimaji zimekuwa zikikamiana sana zinapokutana Majimaji Stadium mjini Songea, mara ya mwisho kukutana, zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 Yanga ikisawazisha kupitia Donald Ngoma baada ya Majimaji kutangulia kwa goli la Peter Mapunda
