STAA WETU:
OBREY CHIRWA: Matunda yake yameanza kuinufaisha Yanga SC. Na Prince Hoza. KATIBU mkuu wa Baraza la wazee la klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali alianza kumponda Obrey Chonda Chirwa akisema si chaguo sahihi kwa Yanga. Yanga iliamua kumsajili Chirwa mwaka jana baada ya kutakiwa kuongeza wachezaji wanne Agosti, ilipofuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika. Beno Kakolanya, Hassan Kessy, Juma Mahadhi na Chirwa ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya kucheza michuano hiyo ya pili kwa ukubwa Afrika kwa vilabu pamoja na kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Yanga ilipangwa kwenye kundi la kifo ambalo alikuwemo bingwa mara mbili wa Ligi ya mabingwa Afrika, TP Mazembe ya DRC, katika kundi hilo pia zilikuwemo Mo Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana. Obrey Chirwa alisajiliwa na Yanga akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, timu ambayo walitokea pia Thabani Scara Kamusoko na Donald Dombo Ngoma ambao wote hao ni wachezaji wa Yanga SC. Hivyo ujio wa Chirwa kwenye kik...