Utawala wa Wallace Karia TFF waandamwa na ufisadi
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Kaimu katibu mkuu wa Shirikisho la kandanda nchini, (TFF), Wilfred Kidau amewajia juu watu wanaosambaza taarifa za uongo mitandaoni kuwa utawala wa Rais mpya wa TFF, Wallace Karia umejiongezea posho.
Kidau amesema taarifa hizo zinasema, wajumbe wa TFF wanajilipa posho shilingi Milioni moja za Kitanzania kwa mwezi wakati Rais akilipwa Milioni sita na makamu wa Rais akilipwa Milioni tano, amedai si kweli na wanapanga kuwafungulia mashitaka watu wanaoeneza uvumi huo.
Ni miezi mitatu tangu Wallace Karia na wenzake waingie madarakani na inadaiwa taarifa zilizosambazwa mitandaoni zinasema, utawala wa Karia umefuta utaratibu ilioukuta wa Jamal Malinzi wa kutojilipa posho
