Machapisho

CHADEMA KWAWAKA MOTO, WAFUASI WA ZITO WAPAMBANA.

Picha
Jeshi la Polisi limewatawanya wafuasi wa Katibu Mkuu wa CHADEMA aliyevuliwa wadhifa Zitto Kabwe na wafuasi watiifu kwa chama hicho waliotaka kupigana baada ya Mahakama Kuu kuhairisha kutoa maamuzi ya kesi iliyofunguliwa na Zitto dhidi ya chama chake. Kutokana na vurugu hizo sasa hali ya hewa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini imeanza kuwa mbaya, jana chama hicho kilitangaza kuwavua uanachama waliokuwa makada wa chama hicho Samosn Mwigamba na Kitila Mkumbo kilichodaiwa kutaka kukisaliti chama hicho. Zito Kabwe ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho alipeleka shauri lake mahakamani la kutaka asivuliwe uanachama ambapo leo hii mahakama ilitangaza kuahirisha kesi hiyo ambapo mapambano kati ya wafuasi wa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini na wale wa chama hicho ambao ni watiifu.

SIMBA HIYOOO ROBO FAINALI MAPINDUZI CUP, YAICHINJA KMKM 1-0.

Picha
SIMBA SC imefanikiwa kufuzu Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMKM usiku wa jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Kwa matokeo hayo, Simba SC inamaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi B, ikiwa na pointi saba, mabao mawili ya kufunga na haijafungwa, nyuma ya KCC ya Uganda yenye pointi saba pia, mabao sita ya kufunga na mawili ya kufungwa. Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao hilo moja likifungwa na Amri Ramadhani Kiemba kwa kichwa, akiunganisha krosi maridadi ya Ali Badru Ali dakika ya tano.

ARSENAL YAPEWA COVENTRY NYUMBANI RAUNDI YA NNE KOMBE LA FA, CHELSEA NA STOKE

Picha
TIMU ya Arsenal itacheza nyumbani mechi ya Raundi ya Nne ya Kombe la FA dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza, Coventry.   Vigogo wote wa Ligi Kuu wametenganishwa katika Raundi hiyo, huku Chelsea ikiwa mwenyeji wa Stoke, wakati mshindi wa mechi ya marudiano kati ya Manchester City na Blackburn atacheza nyumbani na Bristol City au Watford. Stevenage baada ya kuitoa Doncaster watamenyana na washindi mara tano wa Kombe la FA, Everton.

IVO MAPUNDA AANIKA UCHAWI WAKE GOLINI.

Picha
KIPA namba moja wa Simba SC, Ivon Philip Mapunda amesema kwamba kama yupo mchawi anayemfanya afanye vizuri langoni, basi ni Yesu. Akizungumza jana, Ivo alisema kwamba watu wamekuwa wakihisi taulo anayoweka langoni wakati anadaka ni ya kichawi, lakini si kweli ile ni maalum kujifuta jasho wakati anafanya kazi. “Popote ninapokuwa, nakuwa nalindwa na Yesu, timu yoyote nayodakia lango linakuwa salama. Uwezo wangu ni kwa nguvu zake Yesu. Na kwa uwezo wake yeye baba, nitaendelea kufanya vizuri,”alisema. Ivo alifika Uwanja wa Amaan, Zanzibar jana akiwa amevalia fulana yenye ujumbe wa kumsifu Yesu Kristo na akakaa jukwaani wakati Simba SC ikimenyana na KMKM ya Zanzibar na kushinda 1-0, langoni akiwa amesimama kipa mwingine ‘Mfuasi wa Yesu’, Yaw ‘Pastor’ Berko, raia wa Ghana.

MAKALA: NILIJUA TU KAMA ERNIE BRANDTS ATATIMULIWA YANGA.

Picha
Na Prince Hoza KWANZA kabisa ningeanza kuwatakia salamu za mwaka mpya nadhani muda kidogo hatujawasiliana kupitia ukurasa huu, Mwaka 2013 ulikuwa na changamoto zake ambazo kwa namna moja ama nyingine unaweza kusema kuwa haukuwa mzuri katika upande wa michezo. Timu zetu zilizowakilisha nchi hazikufanya vizuri pamoja na timu ya taifa nayo iliendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu, kikubwa tunamshukuru mwenyezi mungu kwa kutupa uzima na hatimaye tuliobahatika kuuona mwaka mpya tunaweza kushuhudia maendeleo katika ulimwengu wa michezo. Licha ya fainali za kombe la dunia ambazo zitafanyika mwaka huu nchini Brazil, pia fainali za Chan nazo zitafanyika mwaka huu nchini Afrika Kusini, Tanzania tutaendelea kuwa watazamaji kufuatia timu yetu ya taifa kushindwa kupata nafasi ya kufuzu. Hata hivyo mwaka jana tulishuhudia klabu ya Yanga ikiliondoa benchi lake la ufundi lililokuwa chini ya Ernie Brandts, kufukuzwa huko kumekuja mara baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-1 na mtani wake wa jadi S...

WENGER AICHEKELEA CARDIFF ISIYO NA KOCHA.

Picha
Arsenal wana nafasi ya kuimarisha uongozi wao wa Ligi ya Premier ya Uingereza ikiwa watawachakaza Cardiff City, ambao hawana meneja, kwa mara ya pili katika kipindi kichache wakati shindano hilo litakapo rejea siku ya kuadhimisha Mwaka Mpya. Ligi ya Premier iko katika pilika pilika za mechi ya nne ndani ya siku kumi wakati ambao wachezaji na vilabu vya nchi zingine barani Uropa viko kwenye mapumziko ya sherehe za Krismasi. Huku ligi hiyo ikiwa imefikia kati musimu huu baada ya raundi 19 kusakatwa, Arsenal wanamiliki uongozi na alama 42, ikiwa ni mara ya kwanza kilabu hicho kuanza mwaka kileleni tangu kampeni ya 2007-08.

HATIMAYE TANGANYIKA IMEREJEA, CCM YAANGUKA.

Picha
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa Rasimu ya Pili ya Katiba ikiwa na mambo sita mapya, huku ikiendelea kupendekeza Muungano wa Serikali tatu na kurejea kwa nchi ya Tanganyika. Rasimu hiyo ya Pili ambayo imetolewa miezi saba baada ya Rasimu ya Kwanza, ilikabidhiwa jana kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam. Akizungumza kabla ya kukabidhi rasimu hiyo, Jaji Warioba alisema ina Ibara 271, tofauti na ile ya kwanza iliyokuwa na Ibara 240.