Vitu vya urithi havikosi kelele

Na Khamis Kilomoni

SIMBA SC sio timu ya mtu au ukoo wa watu fulani.
Naona umetumia nguvu kubwa kuipoka timu ya Simba ingawa sio jambo rahisi kama ulivyodhani maana mamlaka za nchi zinakuzoom tu.

Ulianza kujenga hila kwa kutaka kulazimisha ionekane unaidai SIMBA Tsh 86 billion.

Leo unashupaza shingo kulazimisha mabadiliko yasifanyike kwa hofu ya kupoteza nafasi yako katika Mamlaka za Simba.

Wewe na washauri wako kwa makusudi mnajifanya hamjui kinachoendelea na hamtaki kabisa kusikia mchakato wa mabadiliko unasonga mbele,

Katiba mpya ya Simba haitambui uwepo wa body ya wakurugenzi ambayo kimkakati haina uhalali wa kuendesha shughuli za Simba.

Najiuliza tu, hivi body ya wakurugenzi yenye hisa 49% inapata wapi mamlaka ya kuandaa uchaguzi usiowahusu?
Hiki kinachoendelea ni hatua tu za machawa kujaribu kuwachanganya Wanasimba

Simba sio mali ya mtu binafsi na haiuzwi wala haiwezi kuuzwa iwe mali ya mtu binafsi.
Taratibu za nchi kuhusu uwekezaji lazima zifatwe, simba umeikuta haikuanzishwa na watu wa ukoo wako na hauna haki miliki ya Simba,

Simba ikamilishe mchakato wa Transformation na ikamilishe idadi ya wawekezaji watatu kama mamlaka za nchi zinavyotaka,
Bw Mohammed wewe si ni bilionea ? Kama taratibu za nchi huwezi kuzifuata, anzisha tu timu yako kama Bakhresa , rahisi tu hiyo.

Bw Mohammed umejenga watu wajinga wasioijua kesho bora ya Simba kwa kukuona wewe kama Mungumtu,
Bonus au fedha unazotoa Simba au utulivu uliopo Simba kwa sasa sio kigezo cha kusitisha mchakato wa mabadiliko usiendelee.

Unatengeneza mvutano kupitia Bw Magoli na Mangungu ili Simba ionekane ina mgogoro na watokee watu wawasuluhishe ili bodi yako na mwenyekiti wa Simba waongoze pamoja huku , Bw Magoli akijiweka juu ya uongozi.

Simba inahitaji wawekezaji ili ipate kujiendesha kwa faida zaidi,
Acha kabisa hila za kuizuia Simba isifike kwenye malengi yake,
Simba ni brand kubwa wala sio kwa pesa zako, kama unaamini umeifikisha brand ya Simba kwa pesa yako, anzisha timu yako.

Kuna wakati umenukuliwa ukilaumu mamlaka kama zinakukwamisha vile, *ETI OO MARA TATHMIN, MARA TUNAJADILI"

Huku ukihoji kwanini maamuzi ya wanachama wengi wa Simba yasiheshimiwe?
Yaani maamuzi au mawazo ya watu kama #Mhindi_wa Simba ndio yaheshimiwe?
Hakuna makubaliano yanayokiuka taratibu za nchi yapitishwe tu, kisa eti watu wamekubaliana,

Ujanja wako lazima ufike mwisho,
Simba haiwezi kuendelea na maisha haya haya tangu 2018 huku mnufaika ukiwa ni wewe na unaropika kwa kejeri "ETI UNAPATA HASARA* kaa pembeni wapo wengi wanaoitaka simba wawekeze.

Hili jambo la mchakato lazima likamilike wewe sio mmiliki wa simba , ni mwanachama tu , na mfadhili wa simba maana hata uwekezaji wako ni wakihuni haieleweki umewekeza nini.

#SIMBA_NGUVU_MOJA


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons