Vilabu Afrika vyazidi kujiunga na Umoja wa Injinia Hersi
Umoja wa Vilabu Barani Afrika (African Club Association - ACA) unaendelea kushika kasi kote barani Afrika huku vilabu mbalimbali vikijitokeza na kuthibitisha uanachama wao kufuatia wito wa kufanya soka la Afrika liwe la kibiashara na lenye ufanisi zaidi.
Katika muendelezo wa usajili huo, vilabu vya Tanzania kama Young Africans SC, Azam FC, na Singida Black Stars vipo miongoni mwa orodha ya vilabu vinavyoendelea kurasimisha uanachama wao ndani ya chombo hicho.
Orodha hiyo ya wanachama wanaozidi kujiunga inajumuisha pia miamba mingine ya soka la Afrika kama Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs (Afrika Kusini), Wydad AC, Raja CA na Olympic Safi (Morocco), Al Hilal SC (Sudan), Vipers SC (Uganda), Petro de Luanda (Angola), pamoja na miamba ya Misri kama Al Ahly SC na Red Arrows FC ya Zambia. Kila klabu inayoingia inaongeza nguvu katika ujenzi wa mtandao mpana wa kiushirikiano wa vilabu vya bara hili.
Chini ya uongozi wa Mwenyekiti Injinia Hersi Said {@caamil_88 }, ACA inaendelea kutoa rai na kuhamasisha vilabu vingine vingi zaidi barani Afrika kujiunga ili kujenga sauti moja imara mbele ya CAF na FIFA.
Lengo kuu ni kuhakikisha vilabu vyote wanachama vinanufaika na fursa za kiuchumi, ongezeko la mapato ya matangazo, pamoja na uboreshaji wa miundombinu na utawala bora wa soka.
