Victor Wanyama ainunua Nairobi City
Aliyekuwa nahodha wa Harambee Stars, Victor Wanyama, amechukua umiliki wa klabu ya Nairobi City Stars inayoshiriki Ligi ya National Super League, kutoka kwa mfanyabiashara Jonathan Jackson, na kuwa mmiliki mpya wa klabu hiyo.
Wanyama ana nia ya kuifufua klabu hiyo na kujenga kikosi imara kitakachoweza kushindana, huku hatua hiyo ikimaanisha kurejea kwenye chimbuko la safari yake ya soka.
Kiungo huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur na Celtic aliwahi kuichezea Nairobi City Stars katika miaka yake ya mwanzo ya kucheza soka kabla ya kuanza safari yenye mafanikio makubwa barani Ulaya.
