Simba yatoa dozi mechi ya kirafiki, ikiifunga Madhujaa


Simba SC inaonekana kutokuwa na mchezo kabisa! Kila wanaposhuka dimbani ni kuhakikisha wanaondoka na ushindi, hata kwenye michezo ya kirafiki.

Leo Mnyama alikuwa na kibarua cha kirafiki dhidi ya Mashujaa FC, inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, katika dimba la Mo Arena, Bunju.

Mchezo huo umemalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Bao pekee la ushindi limefungwa na hatari Elie Mpanzu (Jezi namba 34), akimalizia pasi murua kutoka kwa maestro Cletus Chama.

Inaonekana Mnyama bado anaendelea kujenga makali, kuimarisha muunganiko wa kikosi na kujiweka tayari kwa majukumu yaliyo mbele yake.



Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons