Simba yafanya balaa
Timu ya Simba SC au maarufu Wekundu wa Msimbazi, usiku huu wamefanya maajabu na kufanikiwa kuweka rekodi kufuatia kufanya come back na kushinda 3-2 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam dhidi ya Namungo FC.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania bara, ulishuhudia miujiza ya Simba kutoka nyuma kwa mabao 2-1 na kusawazisha na kuongoza na tatu na kuondoka na pointi 3.
Kwa matokeo hayo Simba insfikisha alama 30 katika mechi 10 ikikaa kileleni mwa msimamo wa ligi, mabao ya Simba yamefungwa na Anicet Oura aliyefunga mawili na Rushine De Reuck kwa penalti.Raymond Lulendi, Simba sasa wanaelekea Kenya ambapo watapumzika kufuatia mapumziko ya wiki mbili kupisha timu ya taifa, Taifa Stars kucheza mechi za kimataifa.
