Polisi Kigoma nje Baba Levo Cup
Mbunge wa Kigoma Mjini, Clayton Chipando ambaye pia ni mwanzilishi wa mashindano ya Baba Levo Cup ameamua kuiondoa timu ya Polisi Kigoma kwenye mashindano hayo, kufuatia kukamatwa kwa wachezaji saba wa timu ya Kibirizi FC.
Kupitia taarifa yake, Mbunge huyo amesema mchezo kati ya Polisi Kigoma na Kibirizi FC uliopangwa kuchezwa leo katika mashindano hayo mkoani Kigoma hautafanyika kama ilivyopangwa, baada ya wachezaji saba wa Kibirizi FC kukamatwa tangu jana na kuwekwa mahabusu.
Amesema kutokana na tukio hilo, ameamua kuiondoa Polisi Kigoma kwenye mashindano hayo ili waendelee na majukumu yao ya ulinzi wa taifa.
