Pacome atoa sababu za kufuta picha akiwa Yanga
Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Pacome Zouzoua, ameibua maswali miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo baada ya kufuta picha alizokuwa amepakia kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa amevaa jezi za Young Africans.
Pacome, ambaye kwa muda mrefu amekuwa nje ya uwanja kutokana na jeraha alilopata katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania, bado hajafafanua sababu za kuchukua hatua hiyo.
Hata hivyo, kiungo huyo alionekana uwanjani akiwa jukwaani pamoja na Yao Kouassi Attohoula wakifuatilia mchezo wa Yanga dhidi ya Kagera Sugar, uliomalizika kwa ushindi wa mabao 4-0 kwa Wananchi.
Jambo lingine linalozua maswali ni kwamba, licha ya kufuta picha hizo, Pacome bado hajaondoa utambulisho unaomtambulisha kama mchezaji wa Yanga SC kwenye sehemu ya wasifu (Bio) ya Instagram yake.
Mpaka sasa, haijafahamika sababu halisi iliyomfanya kuchukua hatua hiyo, hivyo mashabiki wa Yanga wanaendelea kusubiri ufafanuzi zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa awali, Yanga imesisitiza kuwa Pacome bado ni mchezaji wa klabu hiyo na anaendelea na mchakato wa kupona jeraha lake licha ya hapo awali Ally Kamwe kukiri kuwa hata kuwa sehemu ya mpango wa timu kwa msimu huu.
