Pacome atimkia Ufaransa

Mchezaji El Professor Pacome Zouzoua Alfajiri Leo, amesafiri kuelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya ‘phase ya 3’ ya matibabu Yake.

Pacome atakaa Ufaransa kwa muda wa wiki nne akipewa matibabu hayo ambapo Gharama zote zimelipwa na Uongozi wa Yanga Chini ya Rais Eng. Hersi Said.

Vile vile, Pacome Zouzoua bado anaendelea kutumikia Mkataba wake na Klabu ya Yanga na analipwa stahiki zake zote kwa mujibu wa mkataba unavyoelekeza ikiwemo na Bonus mbalimbali za ushindi wa Timu.

Ikumbukwe pia, Uongozi wa Yanga chini ya Rais Eng Hersi Said umekuwa mstari wa mbele kuhakikisha unawapatia matibabu bora katika viwango vya juu wachezaji wake pindi wanapopata majeraha.

Hivi karibuni wachezaji Dickson Job na Clement Mzize walimaliza Phase yao ya mwisho wa matibabu nchini Afrika Kusini baada ya upasuaji wa jeraha la Goli lililowakuta nyota hao wawili.

Sambamba na hao, nyota wengine kama Yao Yao, Aboutwaleeb Mshery na Shomari Kibwana waliwahi kusafirishwa nchini Tunisia kwa ajili ya matibabu mbalimbali..


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons