Najifunza kwa Shashaman- Sowah

Mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah, amefunguka kuhusu namna anavyomkubali mshambuliaji wa Yanga SC, Peter Shalulile, akieleza kuwa ni mmoja wa washambuliaji ambao hujifunza kutoka kwao na kuchukua baadhi ya vitu katika mchezo wake.

Sowah ameongeza kuwa kwa mtazamo wake, katika Ligi Kuu ya NBC, Shalulile ndiye mshambuliaji pekee anayempa ushindani, akidai kuwa hakuna mshambuliaji mwingine anayemlinganisha naye katika ligi hiyo.

Kauli hizo amezitoa leo wakati akifanya mahojiano na SOSMEDIA katika siku ya Singida Black Stars Media Day, iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Azam Complex.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons