Mofokeng awaniwa na vilabu vya Ulays

-Nyota wa zamani wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini Relebohile Mofokeng ameingia kwenye rada ya vilabu vikubwa Barani Ulaya baada ya kufanya vizuri na klabu ya Royale Union Saint-Gilloise ya Ubelgiji.

Timu za Lille ya Ufaransa na Bayer Leverkusen ya Ujerumani zimeonesha nia ya kuhitaji saini yake mwezi January.

Mofokeng (22)alijiunga na Saint-Gilloise Julai 2,2026 akitokea Orlando Pirates kwa thamani ya Tsh bilioni 10.4, amecheza jumla ya mechi 14 na kufunga mabao 6 huku akitoa pasi 3 za mabao.

Ukiachana na Lille na Bayer Leverkusen zilizoonesha nia...Chelsea, Atletico Madrid, Napoli na Brighton and Hove Albion zinatajwa kumfuatilia nyota huyo ambaye thamani yake inatajwa kufikia Tsh Bilioni 45.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons