Injinia Hersi aalikwa na FIFA na kuzungumza


Rais wa Yanga SC Injinia Hersi Said ameonesha fahari yake baada ya kualikwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuwasilisha programu rasmi ya mafunzo ya FIFA Diploma in Football Law, katika Module 3 inayofanyika Rabat, Morocco.

Hersi Hersi Said ameeleza kuwa mwaliko huo ni ishara ya imani na heshima anayopewa, sambamba na kutambua maendeleo yaliyofikiwa na klabu yake. Aidha, ameonesha umuhimu wa Afrika kuwa na sauti yenye nguvu katika mijadala na maamuzi yanayohusu mustakabali wa soka la dunia.

Ameishukuru FIFA kwa kumpa jukwaa hilo na kueleza fahari yake ya kuiwakilisha Afrika katika mjadala huo wa kimataifa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons