Infantino aitolea nje Nigeria kuandaa kombe la Dunia

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, amebainisha kuwa kwa sasa taifa la Nigeria halina miundombinu ya kutosha inayokidhi vigezo vya kuandaa fainali za Kombe la Dunia.

Akizungumza kuhusu fursa za uenyeji wa mashindano makubwa barani Afrika, Infantino ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa katika viwanja vya kisasa, usafiri, na huduma nyingine za kijamii ni sharti la msingi kabla ya nchi hiyo kufikiriwa kupewa jukumu hilo zito.

Hata hivyo, kiongozi huyo mkuu wa soka duniani amesisitiza kuwa milango bado iko wazi kwa Nigeria katika siku zijazo endapo itachukua hatua madhubuti za kuboresha mazingira yake ya kimichezo.

Kauli hiyo imeibua mjadala mpana miongoni mwa wadau wa soka nchini humo, wengi wakitaka serikali na shirikisho la soka (NFF) kuweka mipango ya muda mrefu ili siku moja ndoto ya kuleta Kombe la Dunia Afrika Magharibi itimie.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons