Haji Manara atemwa Wasafi FM

Aliyekuwa mtangazaji katika kipindi cha jana na Leo kinacho rushwa na Wasafi Fm Haji Manara, amefukuzwa kazi kwa kile kinachodaiwa ni kukosa maelewano na watangazaji wenzake wa kipindi hicho, Edo Kumwembe na Oscar Oscar.

Kwa mara ya kwanza Kumwembe na Oscar walipeleka malalamiko kwenye uongozi wa Wasafi lakini hawakupewa ushirikiano, wakaenda kwa kumkurugenzi ambaye ni Diamond pia hawakupata ushirikiano.

Awamu hii ya pili walipeleka ombi la kuacha kazi ili wamuachie Manara kipindi lakini uongozi wa Wasafi Media kwa kushirikiana na Diamond wameamua kumpumzisha Haji Manara ndo sababu mpaka sasa Haji Manara haonekani kwenye kipindi cha Jana na Leo pale Wasafi.

Inasemekana ndo sababu Manara hajaonekana kwenye msafara wa Davido kitu ambacho ni tofauti hasa ukizingatia kwenye matukio yote ya kiburudani yanayo mhusu diamond ndani ya nchi manara amekuwa bega kwa bega na Diamond.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons