FPF yakiri Ureno itamheshimu sana Ronaldo
Shirikisho la Soka la Ureno (FPF) limethibitisha rasmi mabadiliko ya muundo wa namba 7 kwenye jezi za timu ya Taifa hilo ili kuheshimu mchango mkubwa wa Cristiano Ronaldo baada ya nyota huyo kutangaza kustaafu soka la kimataifa mnamo Novemba 2026.
Uamuzi huu unahitimisha safari yake ya kihistoria ya miaka 23 akiwa na kikosi hicho, ambapo anaondoka akiwa mfungaji bora wa muda wote wa Ureno kwa rekodi ya mabao 146 katika mechi 234.
Kwa mujibu wa utaratibu huo mpya, wachezaji wengine wataendelea kuvaa jezi namba 7 ya Ureno, lakini muundo halisi wa namba hiyo uliotumiwa na Ronaldo umefungwa rasmi kama kumbukumbu ya heshima kwake.
Tofauti na muundo wa awali uliokuwa na namba 7 iliyonyooka bila mstari wowote wa kukatiza, jezi mpya za Ureno kuanzia sasa zitaweka mstari wa mlalo (cross) katikati ya namba hiyo (7̶).
Hatua hii ya ubunifu imechukuliwa kwa kuwa sheria za mashindano ya kimataifa chini ya FIFA na UEFA haziruhusu timu za taifa kustaafisha kabisa namba 1 hadi 23 kwenye vikosi vyao.
Hivyo, Ureno imebuni mbinu hii ya kubadilisha muonekano wa tarakimu hiyo ili kuhakikisha kuwa hakuna mchezaji mwingine atakayevaa muundo uleule wa namba 7 aliouvaa Ronaldo enzi za uchezaji wake.

