Fadlu ajivunia kikosi

“Sisi ni mabingwa wa Tanzania tuna kikosi kizuri, benchi imara la ufundi na malengo makubwa. Tuna imani na uwezo wetu.

Tumekuwa tukiifuatilia na kuichambua timu pinzani, ikiwemo mchezo wao wa hivi karibuni dhidi ya JS Kabylie.

Kwa kuwa wana kocha mpya, kuna baadhi ya mabadiliko ya kiufundi ambayo tumeyaona, hivyo tunatarajia kukutana na timu yenye mbinu tofauti.

Hata hivyo, jambo kubwa kwetu ni kujiandaa vizuri sisi wenyewe. Tunafanya uchambuzi wa nguvu na udhaifu wetu pamoja na maeneo tunayoweza kuyatumia ili kuongeza ufanisi katika mashambulizi yetu.

Hii ni wiki yetu ya kwanza kuwa na kikosi kizima baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa. Tutaitumia kufanya mazoezi ya kutosha, vikao vya uchambuzi wa video na maandalizi ya kiufundi ili kuhakikisha wachezaji wanakuwa tayari kimwili, kiakili na kisaikolojia.

Ligi ya Mabingwa Afrika ni mashindano yenye ushindani mkubwa, hivyo kila mchezo unahitaji maandalizi na kiwango cha juu cha ushindani.” Fadlu Davids


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons