Djigui Diarra aomba kuondoka Yanga
Mlinda mlango wa Young Africans SC, Djigui Diarra, ameripotiwa kuwasilisha barua rasmi ya kuomba kuondoka ndani ya klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa misimu kadhaa.
Taarifa zinaeleza kuwa Diarra haridhishwi na mazingira na mwenendo wa sasa ndani ya kikosi cha Wananchi, jambo linalomfanya kutafuta changamoto mpya nje ya Jangwani.
Swali kubwa ni je, endapo Diarra ataondoka katika dirisha dogo la usajili la Januari, Yanga SC itaweza kupata mbadala wa kiwango chake
