Diarra aitwa timu ya taifa
Kipa wa klabu ya Young Africans (Yanga SC) ya Tanzania, Djigui Diarra, amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Mali kwa ajili ya Michezo miwili dhidi ya Rwanda ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Kocha wa Mali, Anthony Da Silva, amemtaja Diarra miongoni mwa Makipa watatu walioitwa katika kikosi hicho cha Wachezaji 25.
Kikosi hicho kinajumuisha Wachezaji wanaocheza katika Ligi mbalimbali za Ulaya, akiwemo kiungo Mamadou Sangaré wa Brentford, Amadou Haïdara wa RC Lens na Kamory Doumbia wa Brest.
Katika safu ya ushambuliaji, Kocha huyo amemteua Lassine Sinayoko wa Paris FC, Dorgeles Nene wa Fenerbahçe na Gaoussou Diarra wa Feyenoord.
Mchezo wa kwanza kati ya Mali na Rwanda umepangwa Novemba 13, 2026, huku marudiano yakitarajiwa Novemba 17.
Mali inalenga kupata matokeo mazuri katika michezo hiyo miwili ili kuimarisha nafasi yake katika mbio za kufuzu AFCON 2027.
