Damaro aukana uraia- wa Tanzania
Kiungo wa Singida Black Stars, Mohamed Damaro Camara, ametangaza kuachana na uraia wa Tanzania aliokuwa amepewa kwa Tajnisi, akieleza kuwa uamuzi huo umetokana na sababu binafsi na za kifamilia.
Taarifa hiyo imeibua upya mjadala kuhusu uraia wake na historia ya kuichezea Yanga SC, klabu ambayo aliitumikia na kushiriki katika mafanikio na ubingwa mbalimbali.
YANGA KUPOKONYWA MAKOMBE?
Damaro alipokuwa Yanga, alisajiliwa kama Mtanzania, licha ya taarifa zake kwenye mifumo ya FIFA kuendelea kumtambulisha kama raia wa Guinea. Hali hiyo iliwahi kuibua malalamiko na mjadala mkubwa kuhusu uhalali wa usajili wake.
Sasa, kufuatia uamuzi wake wa kuachana na uraia wa Tanzania, swali kubwa linaibuka:
