CAF yahamia Dar es Salaam

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limehamishia jijini Dar es Salaam, Tanzania, ofisi za uratibu wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, zilizokuwa Nairobi, Kenya.

Uamuzi huo unaifanya Tanzania kuwa kitovu cha shughuli za uratibu wa maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika kwa pamoja nchini Tanzania, Kenya na Uganda mwaka 2027.

Hata hivyo, CAF haijaweka wazi sababu za kuhamisha ofisi hizo kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam.

Hatua hiyo inakuja wakati maandalizi ya mashindano hayo yakiendelea katika mataifa hayo matatu, huku kutokuwepo kwa utulivu ndani ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF) kukitajwa katika baadhi ya taarifa za habari kuwa miongoni mwa mambo yanayoweza kuwa yamechangia mabadiliko hayo. Hata hivyo, sababu hiyo haijathibitishwa rasmi na CAF.

Taarifa zinaeleza kuwa Serikali ya Tanzania imeipatia CAF ofisi katika jengo lenye ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, lililopo eneo la Posta, Dar es Salaam.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons