Akina Mayele wamoto sana kwenye ligi
Jana walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya klabu ya Libyan Stadium na huo sasa unakuwa ni ushindi wao wa 4 katika michezo 4 ya ligi waliyocheza mpaka sasa msimu huu.
Kwenye hiyo michezo 4 wamefanikiwa kufunga mabao 16 huku wakiwa hawajaruhusu bao lolote lile
Mara ya mwisho wanapoteza mchezo, ilikuwa ni April 23 dhidi ya Swehly Club katika mchezo wa ligi kuu,
Baada ya hapo imepita michezo 16 pasi na kufungwa huku wakiwa wamepata sare mara 2 pekee.
Mchezo wao ujao ni dhidi ya Azam FC, wikiendi ijayo
