AFCON yazirudisha uwanja wa Uhuru, Yanga na Azam
Vilabu vya Young Africans (Yanga SC) na Azam FC vinatarajiwa kurejea kutumia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa michezo yao kufuatia Uwanja wa New Amani Complex kuingia kwenye matengenezo.
Rais wa TFF, Wallace Karia, amesema matengenezo hayo yanayohusiana na maandalizi ya AFCON yanatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa Desemba.
Hivyo, Uwanja wa Uhuru utakuwa tena mwenyeji wa michezo ya vigogo hao wa soka nchini wakati kazi za ukarabati zikiendelea.
