Yanga yakubali yaishe, yageukia Ligi ya mabingwa Afrika
Baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya TRA United kuahirishwa, Mabingwa Watetezi Young Africans (Yanga SC) wanahamishia nguvu zao zote kwenye michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League).
Mchezo unaofuata wa Wananchi utakuwa wa Mzunguko wa Kwanza wa Raundi ya Pili ya Kufuzu dhidi ya CFF Andoharanofotsy (CFFA) kutoka nchini Madagascar, utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 17, 2026 majira ya saa 9:00 alasiri (15:00
