Yanga yaamkia Ligi ya mabingwa
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika Dar Young Africans maarufu Yanga SC, jioni ya leo wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CFFA FC ya Madagascar raundi ya kwanza michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika.
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza ulifanyika ugenini ulishuhudiwa Yanga ikipata magoli yote manne ya ‘Wananchi’ wakiwa ugenini Azam Complex, Chamazi; wafungaji ni Cheikh Toure, Albert Kangwanda, Mudathir Yahya na Maxi Nzengeli.
