YANGA WANAOGOPA KUFUNGWA....

Na Prince Hoza Matua

AFISA wa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe aliweka wazi kwamba sababu za timu yake ya Yanga kutaka mchezo wake dhidi ya TRA United ya mkoani Tabora ni kuhofia ya msimu wa mwaka juzi kujirudia.

Jumamosi iliyopita Yanga ilipokea kichapo cha mabao 2-1 toka kwa mahasimu wake Simba SC katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara NBC Primier League.

Kipigo hicho kimesononesha Wanayanga na kuwafanya mashabiki wake kujaa hudhuni huku wengine wakikimbia wanapokaa kuhofia kutaniwa na mashabiki wa Simba.

Lakini pia inaweza kukumbushia ya msimu juzi ambapo timu hiyo ilipoteza michezo mitatu mfululizo, huku michezo miwili ya Ligi Kuu bara na mmoja wa kimataifa.

Kupoteza mchezo mmoja wa kimataifa dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan kilipelekea timu hiyo kutolewa katika hatua ya makundi, Ally Kamwe alikumbusha kwamba Yanga ilifungwa bao 1-0 na Azam FC katika uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Baada ya kipigo hicho, Yanga ilicheza mchezo mwingine katika uwanja wa KMC Complex na timu ya Tabora United sasa TRA United na kufungwa tena kwa jumla ya mabao 3-1.

Kipigo hicho kilisababisha Yanga kumtimua aliyekuwa kocha wake mwenye mafanikio Miguel Angel Gamondi raia wa Argentina ambaye aliifanya Yanga kuwa na makali, uongozi wa timu hiyo uliamua kufanya maamuzi magumu.

Yanga ikahamishia nguvu zake katika michuano ya kimataifa na mchezo uliokuwa mbele yake ni wa Ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi na ikicheza na timu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan.

Mechi hiyo ikipigwa uwanja wa Mkapa Stadium na ikipokea kichapo kingine cha mabao 2-0 na kufifisha matumaini yake ya kusonga mbele,rekodi za msimu juzi zinataka kujirudia msimu huu isitoshe imeanza kwa kipigo cha mabao 2-1.

Kufungwa na mtani wake wa jadi kunauma tena halafu icheze mwingine wa Ligi Kuu bara na TRA United ni kukumbusha machungu.

Uongozi klabu hiyo ukaamua kuisogeza mbele mechi hiyo Ili igeukie mchezo wake wa Ligi ya mabingwa Afrika raundi ya kwanza na timu ya CFFA ya Madagastar.

Endapo Yanga ingecheza na TRA United huenda historia ingejirudia na timu kuharibu tena kwani ingefungwa kwa mara ya pili na baadaye kutishia uwepo wake michuano ya kimataifa.

Nilichogundua mimi anko Hoza kwamba Yanga wanaogopa kufungwa, suala la kufungwa ni marufuku kwa Yanga na ndio maana mashabiki wake wamekimbia vijiwe eanavyokaa.

Na kama siku ile Simba ingeibuka na magoli si chini ya ma- 5 au 6 nadhani kuna watu tusingewaona tena, Yanga hawataki kabisa kufungwa na mchezo wa mpira wa miguu una matokeo ya aina tatu, kushinda, kufungwa na kutoka sare.

ALAMSIKI 


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons