YANGA PRINCESS SIO WAPINZANI WA SIMBA QUEENS
Na Prince Hoza Matua
IMEFIKA wakati tuongee ukweli ti ni sio kuficha ficha ni kwamba upinzani wa Simba na Yanga ubaki kwa timu ya wanaume hasa zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania bara, lakini huku kwingine upinzani umeamuliwe na matokeo.
Hiyo yote imetokekana na matokeo ya mechi yao ya jana ya Ngao ya Jamii iliyochezwa katika uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam, katika mchezo huo Simba Queens iliondoka na ushindi wa mabao 3-0.
Achana na ushindani wao kwenye upande wa wanaume ambao unajulikana kwani kuna wakati Simba inamnyanyasa Yanga na pia Yanga inamnyanyasa Simba.
Ukienda kwenye takwimu zao timu gani insongoza kumfunga mwenzake mara nyingi utaons kila moja imewahi kumfunga mwingine, vipigo vikubwa kama vile kumfunga mwenzake mabao 6, 5, 4 ama 3 zote imewahi kufanya hivyo ingawa Simba ndio iliyowahi kumfunga Yanga mabao 6-0.
Lakini Yanga imewahi kuwafunga
Simba mabao 5 zaidi ya mara moja, ushindani wa Simba na Yanga au Yanga na Simba umekuwa na upinzani wa kweli kwa maana kila mmoja anaweza kumfunga mwenzake.
Oktoba 10 mwaka huu, watani hao wa jadi wanatarajia kukutana tena katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu bara, lakini kwa upande wa dada zao Yanga Princess na Simba Queens haiko hivyo.
Ushindani umekuwa wa upande mmoja hasa kwa Simba Queens kupata ushindi mara kwa mara wanapokutana, Yanga Princess imekuwa timu ya kutimua kocha inapofungwa na Simba Queens.
Nakumbuka katika takwimu zao Simba Queens imekuwa ikimfunga Yanga Princess na mara moja au mbili Yanga Princess ikiibuka na ushindi katika mara zote walizokutana.
Inafikia kwamba wanapokutana tena Simba Queens wanaona kama wanacheza na timu ya kawaida kwa sababu haiwaoi changamoto yoyote kama zilivyo kwa wanaume.
Kuna uwezekano upinzani wa Simba Queens uhamie kwa JKT Queens na si Yanga Princess, Simba ndo wanaonekana wanasajili wachezaji kuliko Yanga Princess.
Mchezaji mpya wa Simba Queens amekuja kuchukua nafasi ya Jentrix Shikangwa ambaye amekwenda kwenye Klabu FC Masal Women huko nchini Misri.
Senaf Demite Mzaliwa wa Ethiopia, ameletwa duniani Kwa ajiri ya kucheza Mpira na kufunga magoli habahatishi wala nini hio ni desturi yake kufunga magoli.
Msimu Jana akiwa na Klabu ya CBE nchini Ethiopia amefunga magoli 14 ndiyo Simba SC kumuona kuwa huyu mshambuliaji ana kitu atawasaidia.
Hili Septemba 30 anacheza mchezo wake wa Kwanza nchini Tanzania akiwa na Uzi wa Simba SC na kufunga Bonge moja la goli tena ameifunga Yanga SC sio Jambo dogo mchezaji ambaye anaonyesha hana presha kabisa na mechi Kubwa kama hizi yeye mpe majukumu atayafanya kitu kingine kizuri kutoka Kwa mshambuliaji huyu ana uwezo wakupiga mashuti na kujaribu ndiyo jadi yake.
Pengine huyu Senaf Demite ana uwezo wakuwapatia Simba SC magoli kumi na kuendelea ndani ya msimu huu 2026/2027, Mungu amuepushie majeraha mchezaji huyu.
ALAMSIKI

