Yanga na TRA United shughuri Jumamosi

Kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha, kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Jumamosi hii, Oktoba 24, 2026 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Yanga imeondoka jijini Dar es Salaam saa chache baada ya kufaulu mtihani wa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kwa kuifunga CFFA mabao 4-1 katika mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Yanga imetinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 8-1, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa mwishoni mwa juma lililopita

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons