Yanga kutupa karata yake leo


​Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Young Africans SC (Yanga SC), wanatupa karata yao muhimu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League) kwa kuvaana na CFFA kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Raundi ya Pili ya Kufuzu leo hii majira ya saa 9:00 alasiri (15:00).

​Wananchi wanaingia kwenye mchezo huu ugenini wakisaka matokeo mazuri yatakayowaweka kwenye nafasi nzuri na kuwapunguzia presha kuelekea mchezo wa marudiano. Kikosi hicho kinaingia uwanjani kikiwa na maandalizi kabambe pamoja na hamasa kubwa ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

​Baada ya kupepetana katika mchezo wa leo, miamba hiyo miwili itarudiana tena katika mzunguko wa pili utakaopigwa siku ya Jumatano, Oktoba 21, majira ya saa 1:00 usiku (19:00) ili kumpata mshindi atakayesonga mbele.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons