Wydad Casablanca kumtambulisha Nabi
Aliyekuwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi, anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa miamba ya soka ya Morocco, Wydad Athletic Club wakati wowote kuanzia sasa.
Kocha huyo raia wa Tunisia amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza muda zaidi, huku akitarajiwa kuwasili jijini Casablanca sambamba na jopo la wasaidizi wake nane.
Ujio wa Nabi ndani ya klabu hiyo, unaelezwa kuwa ni mpango maalum wa kukisuka upya kikosi cha Wydad AC na kukirejesha katika kilele cha mafanikio ndani na nje ya Morocco.
