Spika wa Bunge amaliza bifu la MO Dewji na Haji Manara, sasa njia nyeupe kurudi Simba


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, akimtania Diwani wa Kata ya Kariakoo, Mhe. Haji Manara , kuchukua jukumu la kumaliza mgogoro wake na Rais wa Heshima na Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), baada ya Manara kufanikiwa kumaliza uhasama wa miaka 31 kati ya Madrasa mbili za Kariakoo.

Zungu ameyasema hayo wakati wa hadhara ya Maulid iliyofanyika Msikiti wa Manyema, Ijumaa Oktoba 16, 2026, Jijini Dar es Salaam, huku akidai anaamini Manara ni Mwanasimba hasa na kuwa huko alipo sasa Yanga sio kwa Manara.
.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons