Simba yapoteza tena mchezo Afrika Kusini


Simba SC imepoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Sekhukhune United katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Johannesburg, Afrika Kusini.

Chibuike Ohizu aliifungia Sekhukhune dakika ya 2, kabla ya Elie Mpanzu kusawazisha dakika ya 40 kwa krosi ya Nickson Kibabage.

Dakika ya 74, Sekhukhune walipata bao la pili lililoamua mchezo. Kelvin Nashon alifunga dakika ya 87, lakini bao hilo lilikataliwa na mwamuzi kwa madai ya madhambi yaliyotangulia.

Simba sasa inarejea Dar es Salaam kujiandaa na Dabi ya Kariakoo baada ya kukamilisha kambi yake ya Afrika Kusini.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons