Simba yailalua Yanga
Hatimaye timu ya Simba imeondoa ukame wa kumfunga Yanga, baada ya usiku huu kuifunga Yanga mabao 2-1 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu bara.
Licha ya kuutawala mchezo, lakini vijana wa Yanga walitangulia Kwa bao moja lililofungwa na Petet Shalulile katika dakika ya 5 kipindi cha kwanza kabla ya Neo Maema kusawazisha dakika ya 68.
Elie Mpanzu katika dakika ya 71 aliiandikia Simba bao la pili na kuhitimisha unyonge wa Simba kwa Yanga uliodumu muda mrefu, mara ya mwisho Simba kumfunga Yanga ilikuwa mwaka 2023.
Kwa matokeo hayo Simba imekwea kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 21 huku watani zao Yanga wakishika nafasi ya pili na pointi 18.
