Simba kumrudisha Prince Dube

Tetesi za usajili wa dirisha dogo zinaendelea kuhusishwa na klabu ya Simba SC, huku taarifa kutoka kwa wachambuzi zikidai kuwa klabu hiyo inapanga kufanya mabadiliko katika safu yake ya ushambuliaji kwa kumuondoa Doumbia, anayecheza nafasi ya namba 9.

Katika tetesi nyingine, mshambuliaji wa zamani wa Young Africans, Prince Dube, anatajwa kuwa na mpango wa kurejea Tanzania na kujiunga na wapinzani wao, Simba SC.

Taarifa hizo zinadai kuwa Yanga ilikuwa na nia ya kuendelea kuwa na huduma ya Dube na inadaiwa kumuwekea ofa kubwa, lakini mchezaji huyo anatajwa kuwa na wazo la kurejea Tanzania akiwa na lengo la kuitumikia Simba SC.

Hata hivyo, hadi sasa suala hilo bado ni tetesi za usajili, na hakuna uthibitisho rasmi kuhusu uwezekano wa Dube kujiunga na Simba SC.

Mashabiki wa Simba wanasubiri kuona kama tetesi hizo zitageuka kuwa usajili halisi katika dirisha dogo. Taarifa zaidi zitafuatia kadri hali itakavyoendelea.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons