Rekodi ya Peter Shalulile kuvunjwa Ligi Kuu Afrika Kusini
Kocha wa Stellenbosch FC, Gavin Hunt, amethibitisha kuwa mshambuliaji Bradley Grobler analenga kuvunja rekodi ya ufungaji mabao katika historia ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL).
Grobler mwenye umri wa miaka 38, anahitaji kufunga mabao manne pekee ili kufikia rekodi ya mabao 134 iliyowekwa na Peter Shalulile.
Gavin Hunt alisema:
“Ni wazi kuwa analenga rekodi hiyo, nasi tunatumaini kumsaidia kuifikia. Anatuhitaji, nasi tunamhitaji.”
