Mtanzania atinga nusu fainali Miss World
Historia inaendelea kuandikwa nchini Thailand ambapo mrembo wa Tanzania, Jihan Dimack, amefanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali (Top 4) katika kipengele kikubwa cha ‘Country’s Power of the Year’, akiendelea kuwasha moto kama mwakilishi pekee kutoka bara la Afrika aliyesalia kwenye hatua hiyo ngumu.
Katika vita hii ya kuwania nafasi ya kuingia moja kwa moja hatua ya Top 20 kwenye fainali, Jihan anakabiliana na wapinzani watatu imara ambao ni Shyare Andrade (Miss Grand Ecuador), Ignacia Michelson (Miss Grand Chile), na Emoura Pham (Miss Grand Vietnam).
Raundi ya nne ya upigaji kura imefunguliwa rasmi leo Oktoba 2, 2026, na itafungwa Oktoba 4, 2026, hivyo huu ni wakati wetu kama nchi kuonyesha nguvu kwa pamoja na kumvusha Jihan kwenda fainali.
