Mr Blue aelezea kilichomtoa kwa Dudubaya
Mr Blue amesema kuwa wakati yupo kwenye lebo ya Dudu Baya Foundation alipata idea ya wimbo wa Gari la Baba lakini kwa bahati mbaya alipompelekea Dudu Baya aliukataa wimbo huo na kumtaka aandike idea nyingine ya mpangaji.
Mr Blue amesema kuwa kwenye idea ya Gari la Baba ilikuwa rahisi kuitengeneza kuliko mpangaji kwasababu kwa wakati huo hakuwahi kupanga hivyo akaona jambo limekuwa gumu akaamua kutoka kwenye lebo moja kwa moja.
''Baba yangu alikuwa na gari upande wa baba yangu walikuwa matajiri nipata idea naingia na gari la baba nilipompelekea dudu baya akaniambia baba yako anagari akaniambia katengeneze ngoma nyingine inaitwa mpangaji mimi sijawahi panga nyumba na dudu baya foundation nikatoka''Amesema -Mr Blue
