Motsepe athibitisha hii ni awamu yake ya mwisho CAF


Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe, amethibitisha kuwa awamu yake ya sasa ndiyo ya mwisho akiwa kama mkuu wa shirikisho hilo. ⚽👏

Motsepe alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mnamo Machi 12, 2021. Baadaye alichaguliwa tena bila kupingwa mnamo Machi 12, 2025, kwa awamu ya pili ya miaka minne inayodumu hadi Machi 2029.

Na hivi sasa Motsepe tayari amethibitisha kuwa hatowania tena nafasi hiyo kwa awamu ya tatu na atang'atuka madarakani mara tu awamu yake ya sasa itakapokamilika mwaka huo wa 2029.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons