Mayele aonesha pasipoti zake tatu
Nyota wa DR Congo na mshambuliaji wa Al Ahli Tripoli ya Libya, Fiston Mayele, ameonyesha pasipoti zake mbalimbali alizonazo hivi sasa:
Pasipoti ya kawaida ya DR Congo
Pasipoti ya utumishi (Service Passport)
Pasipoti ya kidiplomasia, baada ya kutunukiwa cheo cha Knight (Fundi/Askari wa Heshima)
Mshambuliaji huyo wa DR Congo, ambaye aliiwakilisha nchi yake katika Kombe la Dunia, sasa amerejea Libya kuendelea na msimu akiwa na pasipoti mpya ya kidiplomasia.
