Manqoba amsifia Chuga

Kocha Manqoba amesema kuwa Chuga Boy ni mchezaji wake ambaye anapohitaji matokeo, anayapata kwa haraka zaidi. Amesema ni tofauti na wachezaji wengine wadogo, kwani anapowekwa kwenye mfumo ana uwezo wa kubadili mchezo ndani ya dakika chache.

Manqoba anadai kuwa Chuga Boy alianza kumpa matumaini kwenye mchezo wa dabi dhidi ya Simba SC, baada ya kupewa dakika chache tu lakini akaonyesha makubwa uwanjani. Amesema kwa sasa ataanza kudili na wachezaji wadogo wenye mvuto zaidi pamoja na kasi kubwa kwenye mechi zinazofuata.

“Chuga anajua kutuliza mpira na kuondoa presha mapema pindi tu anapofika eneo la hatari. Anatoa pasi zinazofika bila kuwa na changamoto yoyote, hiyo inanipa nafasi ya kufanya hesabu zangu sawa.”


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons