Manqoba aanza visingizio kuhusu kipigo cha Simba

kocha mkuu wa Young Africans MANQOBA, anadai kuwa kama wachezaji wake wasingepigwa kadi nyekundu kwenye mechi za nyuma, pamoja na kuwa na majeraha, Simba walikuwa ni wachache sana.

Anadai kuwa Aziz Ki hakuwa kwenye mfumo, Selemani Mwalimu hakuwa kwenye mfumo pia. Hata Yao Yao pia alicheza, ila kipindi cha pili alipotoka, pengo liliweza kuonekana. Anasema ubaya wa mchezo huu, tulitawala dakika za mwanzo tu, ila kipindi cha pili sababu zangu hazikwenda sawa.

“Mchezaji kama Chuga Boy ni mchezaji mdogo sana kiasi kwamba alipata presha ya mchezo, jambo ambalo lilipelekea kuanza kulinda kuliko kushambulia. Mchezo umekamilika, lakini matokeo hayajanipa ushawishi kabisa. Tusubiri mechi zinazofuata, nitafanya makubwa zaidi. Asante.”

— Kocha wa Young Africans, Manqoba Mngqithi



Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons