Libasse kuikosa Yanga Okt 10
Taarifa zinasema mshambuliaji wa Simba SC, Libasse Gueye, yuko hatarini kuwa nje ya uwanja kwa wiki nne hadi tano kufuatia majeraha ya kifundo cha mguu.
Ripoti hizo zisizo rasmi zinaeleza kuwa maumivu hayo yanaweza kumfanya akose mchezo wa Dabi ya Kariakoo, huku Kocha Mkuu Steve Barker akitaja kuanza kumwandaa Keltso kama mbadala wake katika safu ya ushambuliaji.
Wadau, Libasse akikosekana kwenye Dabi mtaambia nini watu?
