Kocha wa zamani Simba aula Tunisia

Kocha wa zamani wa Simba SC, Pablo Franco Martin ametangazwa kama kocha mkuu mpya wa klabu ya Espérance Sportive de Tunis ya Tunisia baada ya kuachana na Mabingwa wa Ligi kuu Morocco, Maghreb de Fès.

Pablo 46 ambaye aliiongoza MAS Fès kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchini Morocco msimu wa 2025/26 amesaini mkataba wa kuitumikia Esperance Dr Tunis mpaka mwisho wa msimu wa 2026/27 na chaguo la ongezeko la muda wa utumishi wake kulingana na matokeo.

Kocha huyo aliyeifundisha Simba SC kwa msimu mmoja kuanzia Novemba 2021 mpaka Mei 2022 alikuwa kocha wa kwanza kuipatia MAS Fès ubingwa wa Botola Pro kwa mara ya kwanza baada ya miaka 41 na anachukua mikoba ya kocha Laurențiu Reghecampf aliyeondoka Athletic Taraji mnamo Septemba 2026.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons