Kocha msaidizi Kagera Sugar afariki

Uongozi wa klabu ya Pamba Jiji FC umetangaza kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Themi Felix, kilichotokea leo katika Hospitali ya Bugando alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kupitia taarifa yake ya leo Oktoba 17, 2026 Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Pamba Jiji FC, ametoa pole kwa familia, ndugu, na mashabiki wote huku akieleza kuwa kifo chake ni pigo kubwa na pengo lisilozibika kwa klabu hiyo na soka kwa ujumla kutokana na mchango, weledi, na jitihada zake.

Aidha uongozi wa klabu hiyo umeeleza kuwa taratibu za msiba na mazishi zitatangazwa baada ya kukutana na familia ya marehemu huku akiwaomba mashabiki, wadau, na wote walioguswa na msiba huo kuwa watulivu na kuiombea familia ya marehemu nguvu na uvumilivu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons