Kamungo apata pasipoti ya Tanzania
Mchezaji Mtanzania Bernard Kamungo ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Congo DR hatimaye amepata hati ya kusafiria ya Tanzania na sasa ataanza kuitumikia Taifa Stars. Kamungo alishindwa kucheza kwenye mchezo kati ya Tanzania na Guinea Bissau pale Amaan Zanzibar kwakuwa hakuwa na passport, mchezo ambao Stars ilichapwa 2-0 nyumbani.
