JKT Tanzania yailaza Mbeya City
Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Maafande wa JKT Tanzania dhidi ya Mbeya City umetamatika katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam, ambapo JKT wameondoka na ushindi wa 2-1 na kuzibakisha alama tatu nyumbani.
Magoli ya JKT Tanzania yamefungwa na Valentino Mashaka 45+2’ na Fredrick Magata 90’, huku goli la Mbeya City likifungwa na Joseph Mbaga 90+4’.
