Jean Baleke awajia juu washambuliaji Simba
Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba SC na Yanga SC, Jean Baleke, amezua mjadala kwenye ulimwengu wa soka nchini baada ya kutoa kauli ya kujiamini na kuponda safu ya ushambuliaji ya sasa ya Simba SC.
Jean Baleke anasema tangu alipoondoka Simba yeye pamoja na Moses Phiri bado hajaona mshambuliaji bora wa kumfikia ndani ya Simba.
Kwa mujibu wa Baleke maana yake hawa wote hawamuwezi:
Fredy Fungafunga ❌ Jobe ❌ Ateba ❌ Mukwala ❌ Mgunda ❌ Doumbia ❌ Mwalimu ❌ Sowah ❌"
